BOBAN, TAITA SI PENGO KILI STARS-JULIO


KOCHA Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars', Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kutokuwepo kundini kwa nyota wawili wa timu hiyo waliotimuliwa kwa utovu wa nidhamu, Haruna Moshi 'Boban' na Godfrey Taita, si pengo kwa timu hiyo.
Julio alisema wachezaji wote waliomo ndani ya kikosi hicho ni bora hivyo kama hao wameoondolewa waliopo wataendelea majukumu yao kama kawaida na hilo limedhihirika hata jana ambapo timu yake iliweza kutinga hatua ya Nusu Fainali ya michuano ya Chalenji.

"Ndiyo maana ya kuwa na wachezaji wengi, tumeita wachezaji ambao tunaamini wana viwango vya hali ya juu, kama kuna waliotoka timu haiwezi kusambaratika ama kushindwa kutimiza wajibu wake, nadhani tuna wachezaji wazuri na ndiyo maana tumefika hatua tuliyofika,"Alisema.

Timu hiyo ambayo ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo, inatarajia kushuka leo katika dimba kukwaana na Uganda Cranes.

Comments

Post a Comment