AYEW, KEITA NA TOURE WATINGA FAINALI TUZO ZA MWANASOKA BORA WA CAF

SHIRIKISHO la soka barani Africa (CAF) limetangaza majina ya wachezaji watatu ambao wametinga fainali ya tuzo ya mchezaji bora kwa mwaka 2011 inayotolewa na Shirikisho hilo. 
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na CAF, mshindi atapatikana kupitia kura ambazo zitapigwa na makocha/wakurugenzi wa ufundi wa wanachama wa CAF, huku hafla ya utoaji tuzo ikitarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa Banquet, Ikulu ya Ghana iliyopo katika jiji la Accra.
Wachezaji hao ni pamoja na (a) Andre Ayew (Olympique Marseille na  Ghana)
(b) Seydou Keita (Barcelona  na  Mali)
(c) Yaya Toure (Manchester City na Cote d’Ivoire)

Comments