ADHABU YAMSUBIRI FABREGAS WA BONGO, GUMBO ATEMWA

ADHABU inamsubiri kwa hamu kiungo wa kimtaifa wa Yanga, Mnyarwanda Haruna Niyonzima 'Fabregas' kutokana na kuchelewa kurejea nchini tangu alipokwenda kwao kwa mapumziko baada ya ada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Chalenji.
Kocha mkuu wa Yanga Kostadin Papic amesema kuwa nyota huyo amekuwa akitoa visingizio mbalimbali ikiwamo  matatizo ya hati yake ya kusafiria ambayo hayanba mantiki yoyote.

"Nitamwadhibu na kumtaka mshahara wake ili iwe fundisho kwa wengine," alisema Papic.
     
Katika hatua nyingine Papic alisema kuwa ametuma majina ya wachezaji 28 kwa ajili ya mashindano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na kumtema kiungo wake, Rashidi Gumbo kutokana na ukweli kwamba hayupo  tayari kwa mashindano hayo.

Comments