25 WAITWA TWIGA STARS KUIKABILI NAMIBIA

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars), Charles Boniface Mkwasa leo (Desemba 16 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la mataifa ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Namibia.
Mechi ya kwanza itachezwa jijini Windhoek, Namibia kati ya Januari 14 na 15 mwaka huu, na ile ya marudiano itachezwa Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu itaanza mazoezi Desemba 19 mwaka huu kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Wachezaji waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti ofisi za TFF siku hiyo saa 9 alasiri tayari kwa kuanza mazoezi.
Wachezaji walioitwa ni Sophia Mwasikili (Sayari Women), Fatuma Bushiri (Simba Queens), Fatuma Omari (Sayari Women), Mwajuma Abdallah (JKT), Asha Rashid (Mburahati Queens), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Ettoe Mlenzi (JKT), Zena Khamis (Mburahati Queens), Fatuma Khatib (Mburahati Queens), Maimuna Said (JKT), Fadhila Hamad (Uzuri Queens), Fatuma Mustapha (Sayari Women) na Evelyn Senkubo (Mburahati Queens).
Rukia Hamisi (Sayari Women), Mwapewa Mtumwa (Evergreen), Judith Hassan (TMK), Aziza Mwadini (Zanzibar), Sabai Yusuf (Zanzibar), Semeni Abeid (Tanzanite Queens), Zena Said (Uzuri Queens), Pulkaria Charaji (Sayari Women), Tatu Said (Makongo Sekondari), Mwanaidi Hamisi (Uzuri Queens), Hanifa Idd (Uzuri Queens) na Fatuma Gotagota (Mburahati Queens).

Comments