ZANZIBAR WATISHIA KUJITOA CHALENJI 2011


CHAMA cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kimetishia kujitoa kwenye michuano ya Tusker Chalenji Cup iwapo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litakwamisha nyota wake wanne waliomo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kujiunga na wenzao waliopiga kambi nchini Misri kujiwinda na michuano hiyo.

Tishio hilo la ZFA limekuja siku chache baada ya ZFA kuiandikia barua TFF, kutaka iwape hati za kusafiria za wachezaji hao ambao ni kipa Mwadini Ally, Nadir Haroub ‘Canavaro’ na Aggrey Morris  ili iwaombee visa lakini tayari kwa safari hiyo lakini hadi jana walikuwa hawajafanya hivyo huku safari yao ikiwa imepangwa kuwa kesho.
 Nyota hao leo walikuwa wanakabiliwa na jukumu la kulitumikia Taifa ambako Taifa Stars ilikuwa ikichuana na Chad kwenye mchezo wa kusaka tiketi kufuzu makundi ya kombe la Dunia.
 ZFA ilikuwa inazihitaji hati za kusafiria za wachezaji hao ili iwaombee visa kwenye ubalozi mdogo wa Misri Visiwani humo lakini TFF imetia pamba masikio, hivyo  nyota hao wakikwama kukwea pipa kesho kwenda Misri, Zanzibar Heroes itajitoa kwenye Chalenji na TFF itawajibika kulipa gharama za tiketi ambazo ni dola za Kimarekani 4200.
Zanzibar Heroes imepiga kambini ya wiki mbili nchini Misri kujiwinda na michuano hiyo ambako inatarajia kurejea Visiwani Zanzibar Novemba 21 kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam kwa kindumbwendumbwe hicho ambacho kinavuta hisia za mashabiki wengi wa soka.

Comments