TFF YASALIMU AMRI YA VILABU

HATIMAYE shirikisho la soka Tanzania (TFF) limesalimu amri ya vilabu vya ligi kuu na ligi daraja la daraja la kwanza kutaka ligi hiyo kuanzia mwakani isimamiwe na kampuni badala ya shirikisho hilo.
Uamuzi huo wa faraja kwa vilabu hivyo, umepitishwa  leo katika kikao baina ya TFF na wawakilishi wa vilabu hivyo uliofanyika kwenye ofisi za TFF.
 Mwenyekiti wa kamati ya mpito ya mchakato wa kuanzishwa kwa kampuni ya kusimamia ligi hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema wanashukuru kufikiwa kwa muafaka juu ya suala hilo.

Comments