TFF YAMSAFISHA MICHAEL WAMBURA

MICHAEL WAMBURA


KAMATI ya rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemsafisha aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha soka mkoani Mara (FAM),kabla ya kuenguliwa kwa madai ya kutokuwa muadilifu, Michael Richard Wambura.
Kamati hiyo hiyo chini ya mwenyekiti wake, Profesa Mgongo Fimbo ilikutana juzi jijini Dar es Salaam na kupitia rufani iliyowasilishwa na Wambura baada ya kuenguliwa na kutoa maamuzi yake.
“Mrufani Bwana Wambura alienguliwa kimakosa na kamati ya Uchaguzi ya TFF na alistahili kugombea nafasi ya uenyekiti wa FAM”, Ilieleza taarifa hivyo.
Hata hivyo, kamati hiyo imeeleza kuwa kwa vile uchaguzi umepita na viongozi kuanza kutumikia chombo chao, kamati ya Rufaa imesita kuwa uchaguzi huo urudiwe ukimjumuisha mrufani.
Kamati hiyo ilipokea rufaa hiyo baada ya Wambura kuenguliwa na kamati ua uchaguzi ya TFF na kisha kukwama rufaa yake katika kamati ya Nidhamu ya TFF na baadaye maahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa masuala ya michezo (CAS).
Kabla ya maamuzi hayo kutolewa na kamati hiyo,kamati ya Rufaa iliridhika kuwa inayo mamlaka kamili ya kusikiliza rufaaa hii chini ya ibara ya 47(4) ya Katiba ya Tff.
“Kwa mujibu wa ibara hii na ibara ya 118 ya FIFA, kamati ya Rufaa inayo mamlaka ya kusikiliza rufaa zote toka kwenye kamati ya Nidhamu isipokuwa pale ambapo kamati ya Nidhamu imetoa adhabu ya onyo, onyo kali au kumsimamisha mhusika chini ya mechi tatu,”Alieleza Fimbo.li
Fimbo ameeleza kuwa, kamati yake inamamlaka mapana kuhusu nidhamu chini ya ibara ya 46 (2) ya katiba ya TFF na kwamujibu wa ibara ya 46 (4) kamati ya nidhamu inaweza kutoa adhabu yoyote iliyoainishwa kwenye ibara ya 45 ya katiba ya TFF na kanuni za adhabu za FIFA.
“IBara hii haimfungi mlalamikaji juu ya namna ya kuifikia kamati hiii;anaweza kuwasilisha malalamiko kwa maandishi au kwa mdomo, iwe rufaa au vinginevyo.Mtu anaweza kujiuliza iowapo kanuni zilizotengenezwa chini ya katiba hii ya TFF zinaweza kubana mamlaka haya ya kamati ya nidhamu.Kwa leo hatulazimiki kulijibu swali hili kama itavyoonekana,”Aliongeza Fimbo.

Comments