TENGA APATA MPINZANI UCHAGUZI CECAFA

MWENYEKITI wa baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) amepata mpinzani katika uchaguzi wa baraza hilo unaotarajiwa kufanyiika Novemba 24, jijini Dar es Salaam.
 Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura  amemtaja mpinzani huyo wa Tenga Fadoul Hussein wa Djibout ambaye ni makamu mwenyekiti wa baraza hilo.
 Alisema mbali na nafasi hiyo, nafasi ya wajumbe wanne wa mkutano mkuu itakayotoa wajumbe wanne, mpaka sasa wamejitokeza watu nane kutoka nchi tofauti ikiwemo Kenya, Somalia, Burundi, Rwanda, Zanzibar, Ethiopia na Tanzania.
 Tenga ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amekalia  nafasi hiyo tangu mwaka 2007, pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Katika uchaguzi huo wajumbe wapatao 11 kutoka nchi wanachama wa Baraza hilo, watachagua viongozi watakaokaa madarakani kwa miaka minne.
mwisho

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHNovember 5, 2011 at 6:59 AM

    YANI HUYO MSOMALI AJE AMSHINDIE TENGA HAPO HAPO NYUMBANI NA NYIE MPO!!!NTAWATAPIKA ILE MBAYA!

    ReplyDelete

Post a Comment