TANGAZO LA SHUKRAN

                 

                                                                            JUMA PENZA
Familia ya Juma Penza ya Gongo la Mboto Dar es Salaam inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshirikiana nasi katika kufanikisha shughuli za msiba wa baba yetu mpendwa, aliyefariki dunia tarehe 12/10/2011 katika hospitali ya Hindu Mandal na kuzikwa tarehe 13/11/2011 katika makaburi ya Kisutu.
Tunatoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. J.M. Kikwete, CCM Makao Makuu, ndugu, jamaa, majirani na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali na kwa namna mlivyoshiriki katika shughuli zote za mazishi. Shukrani za pekee ziwaendee Dr. Macha Ocean Road , wauguzi na madaktari wa Hindu Mandal.
Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu kipee, tunaomba shukrani hizi mzipokee wote kwa mikono miwili kutokana na jinsi mlivyohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli nzima ya msiba wa baba yetu mpendwa Mzee JP.
Tunawashukuru kwa jinsi mlivyokuwa karibu nasi kwa dua nas msombi wakati wote hadi tulipompumzisha baba yetu kipenzi .
Vilevile tunapenda kuwakaribisha katika mkesha wa dua itakayofanyika Ijumaa usiku Novemba 18 kuamkia siku ya Jumamosi Novemba 19 ambapo khitma itasomwa nyumbani kwa marehemu Gongo la Mboto Dar es es Salaam wote mnakaribishwa .
Tunawakaribisha wote kwenye Arobaini ya marehemu. Mkesha na kisomo utafanyika siku ya Ijumaa tarehe 18/11/2011 na kufuatiwa na Khitma itakayosomwa Jumamosi tarehe 19/11/2011 kuanzia saa 5:00 asubuhi nyumbani kwa marehemu Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam.
Inna lilah Wainna Ilaih Rajiun

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHNovember 17, 2011 at 8:39 PM

    INNALILAHI WAINA ILLAIHI RAJOON!MZEE JUMA PENZA KUMBE ALIFARIKI MASKINI!HAWA NDIO WALIOJITOA YANGA NA MAREHEMU MZEE MANGARA TABU KWENDA KUANZISHA PAN!ALIKUA PAN KUFA MTU HUYU MZEE NA NDIO WALIOKUWA WAKIMSAIDIA SANA MANGARA KUIENDESHA PAN AFRICA!WATU WA MJINI WANAZIDI KWISHA JAMANI!NIMESIKITIKA SANA KWA KWELI,MAANA NIMEIKUMBUKA KARIAKOO YETU ENZI HIZO,WAPI "DOZA
    "JABALI LA MUZIKI MARIJANI RAJABU MZEE WA SOMARI STREET GEREZANI KARIAKOO R.I.P. brother,wapi HASSAN OMARI A.K.A.HASSAN TOLOLI MZEE WA SAIGON CLUB KARIAKOO,MTOTO WA NYAMWEZI STREET,R.I.P.Brother,WAPI MANSOOR MAGRAM MZEE WA SAIGON CLUB KARIAKOO,R.I.P. BROTHER,WAPI DITOPILE MZUZURI A.K.A.KAKA DITTO MZEE WA SAIGON CLUB,R.I.P.KAKA! KARIAKOO INAKWISHA JAMANI EEEH!NAILILIA KARIAKOO YETU!NAILILIA SAIGON YETU,KAKANGU ADEN RAGE SAIGON YETU INAKWISHA KAKA!

    SAYZ MDAU WA YANGA BOMBA,MICHIGAN,USA!

    ReplyDelete

Post a Comment