TAMASHA LA UTAMBULISHO WA ALBAMU YA SIFA ZIVUME NOV.27

TAMASHA la kusifu na kumuabudu Mungu lijulikanalo kama ‘Sifa Zivume’ linatarajiwa kufanyika jumapili ya Novemba 27 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
 
Mratibu wa tamasha hilo, Safari Paulo aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba, tamasha hilo litaambatana na uzinduzi wa albamu ya pili ya kwaya ya Rivers of Life iitwayo ‘Sifa Zivume’.

Alisema albamu hiyo imebeba ujumbe wa kubadili maisha ya watu na kuwapa matumaini,huku ikirekodiwa kwa ubora wa hali ya juu wenye kukidhi viwango vya kimataifa, ndani yake kuna nyimbo 15.

Aliongeza kuwa, ndani ya tamasha hilo ambalo litaambatana na maombi ya kumshukuru mungu kwa kufikisha miaka 50 ya Uhuru, kutapambwa na wasanii kama The Voice, Brother Joshua, Victor Aron, Faith Singers na wengineo.

Safari alizitaja nyimbo zilizomo ni pamoja na Elshadai, Tunakushukuru, Mataifa Yatetemeke, Twakuabudu, Mungu Wetu, Wewe Watosha, Hili ni Ombi Langu, You are a lord, Twakuabudu, By the Grace, Hakuna Mungu, I want to See You, Itabibu na Ebenenza.

“Utayarishwaji wa DVD ya albamu hii umekidhi viwango vya kimataifa huku ikirekodiwa live maeneo ya Mlimani City, hivyo nawaomba watu kujitokeza kwa wingi katika tamasha hili ili kuweza kuabudu pamoja”, Alisema.

Comments