SWAHILI FASHION WEEK YAANZA LEO

WAKATI maonyesho ya mavazi ya nne ya ‘Swahili Fashion Week’ ikianza leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa,zaidi ya wabunifu 50 kutoka nchi 11 za Afrika wamejitokeza kushiriki maonyesho hayo.

Mwandaaji wa maonyesho hayo Mustafa Hassanali alisema kwamba lengo la maonyesho hayo ni kukuza mavazi ya Kiafrika.
Alisema kwa kuwa Tanzania mwaka huu inaadhimisha miaka 50 ya Uhuru wameona ni vema kupanua wigo wa maonyesho hao kwa kushirikisha wabunifu wengi zaidi.

Comments