STARS YAFUZU KWA BAHATI

TIMU ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefanikiwa  kufuzu hatua ya makundi ya kuwania kucheza fainali za kombe la Dunia zitakazopigwa Brazil mwaka 2014  baada ya kuisukumiza Chad. 
Stars imejipatia pointi nne dhidi ya tatu walizozipata Chad ambayo jana iliirarua Stars bao 1-0 katika mechi ya marudiano iliyopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
 Katika mechi ya awali Stars ilibamiza Chad mabao 2-1 katika mchezo wa awali uliopigwa N’djamena ijumaa iliyopita.
Kwa kufuzu hatua hiyo, Stars itakuwa kundi moja na Gambia, Morocco na Ivory Coast ambapo itaanza kampeni hiyo mwezi juni mwakani kwa kukwaana na Ivory Coast.
Katika mechi  hiyo, Stars itabaki ikijilaumu kwa kushindwa kuzitumia vema nafasi za wazi ambapo kama washambuliaji wake wangekuwa makini wangecheka na nyavu zaidi ya mara tano.

Comments