SIMBA YATWAA UBINGWA UHAI CHUP

MICHUANO ya soka ya vijana chini ya miaka 20,  ‘Uhai Cup’ imefikia tamati leo ambapo vijana wa  Simba wamefanikiwa kutwaa ubingwa  baada ya kufunga  Azam FC kwa penalti 6-5, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo zilimaliza dakika 90 bila kufungana na hata mwamuzi alipoongeza dakika 30 ambapo nazo zilimalika kwa sare tasa pia na ndipo kuamuliwa changamoto ya mikwaju ya penalti.
Mchezaji bora ni  Ramadhani Singano wa Simba, kocha bora ni Suleiman Matola,mchezaji bora alikuwa  Simon Mzava wa Azam, mwamuzi bora ni  Juma Seifu,  mfungaji bora Willian Luciana wa Simba,kipa bora ni Aishi Salum wa Azam.
Nafasi ya tatu imekwenda kwa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17, (U-17) Sarengeti Boys waliyoipata baada ya  kuifunga Toto African ya Mwanza mabao 2-1.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHNovember 27, 2011 at 6:55 PM

    ANGALAU SASA KINA ADEN WAMEPATA TAJI MOJA TOKA WAINGIE MADARAKANI!

    ReplyDelete

Post a Comment