SIMBA WAMTIMUA BASENA KWA BARUA PEPE

IMEONA isiwe tabu, badala ya kusubiri arejee jijini Simba imetumia barua pepe kocha wake mkuu, Moses Basena ikimjulisha rasmi kutimuliwa kwake.
Maamuzi hayo mazito yalifikiwa na viongozi wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo waliokutana hivi karibuni kujadili mustakabali mzima wa klabu hiyio.
Taarifa zinasema kuwa, baada ya kupitishwa maazimio hayo sasa wapo katika mchakatio wa kusaka kocha mpya huku nafasi zikiwa kwa makocha kutoka Serbia na Ujerumani.( Na Mdau, Somoe Ng'itu-Nipashe).

Comments

  1. Tatizo la Simba sio kocha bali nii uongozi usio shirikishi. Wakati Hassan Dalali akiwa mwenyekiti Simba haikufungwa na Yanga kirahisi hivyo lakini sasa ni kama mchezo. Kwa nini watu kama huyo mzee na timu yake wasiingizwe kwenye kamati ya mashindano ya klabu? Au kigezo cha form iv kinafika hadi katika kamati? Rage hana historia nzuri na ushindi wa Simba na nakuhakikishia hakuna kikombe chochote mtakachopata chini ya uongozi wake. Haiingii akilini kocha mzuri kama Phiri afukuzwe kazi tena kwa sababu za kijinga. Iweni makini ndugu zangu ila ubingwa hamtaupata. Ndio ukweli japo inauma. Vinginevyo hao wazee wapewe nafasi fulani fulani kwenye kamati

    ReplyDelete
  2. Hapakuwa na haja ya kumtimua kocha. Tatizo la Simba ni hiyo kamati ya utendaji chini ya Rage. Badala ya kumfukuza kocha wangekaa chini na kutafakari tatizo liko wapi. Mwaka jana kabla ya mechi tano Simba ilikuwa inaongoza ligi katika kiwango ambacho hakuna aliyeamini kwamba wataukosa ubingwa lakini thats what happened. Matokeo kocha katimuliwa! Mwaka huu wameanza vyema but now wako reachable! Matokeo fukuza kocha. Makocha wangapi watakuja? Tatizo ni uongozi. Hawashirikishi wazee. Before uongozi huu tulikuwa tunapata raha kila mechi hususan against Yanga but under this leaders tunaona aibu mtaani. Hakuna ubingwa mwaka huu hata aje Fergurson. Leta wale wazee kwenye kamati kama ilivyokuwa wakati wa kombe la mapinduzi. Acheni ubinafsi hamtafika popote

    ReplyDelete
  3. YANGA BOMBA - UHURU BRANCHNovember 22, 2011 at 6:33 PM

    MIMI NILISEMA HAPA WAKAJIDAI KUKANUSHA KIKO WAPI SASA?HAWA JAMAA KILE KIPIGO BADO KINAWALEVYA NA BADO!

    ADEN ALIKUA ANAMPONDA YULE MSEMAJI WAO WA ZAMANI KUANDIKA BARUA YA KUACHA KAZI KWA NJIA YA BARUA PEPE NAE AMERUDIA YALEYALE!

    ReplyDelete

Post a Comment