SIMBA SC NA BIRTHDA YA MIAKA 75

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba wanatarajiwa kufanya sherehe maaluim ya kuadhimisha miaka 75 tangu kuanbzishwa kwa klabu hiyo.
Maadhimisho hayo ambayo yataambatana na shamrashamra za kila aina, yanatarajiwa kufanyika mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Chalenji itakayoanza Novemba 25 hadi  Desemba 10 jijini Dar es Salaam.
Moja ya shamrashamra za maadhimisho hayo ni mechi ya kimataifa ya kirafiki baina ya wekundu hao na timu moja kjutoka nje ya nchi, ikiwemo Asante Kotoko
Pia kutakuwa na kisomo maalum kwa ajili ya kuwarehemu wadau wote wa timu hiyo waliotangulia mbele ya haki.

Comments