SIKU CHACHE KABLA YA KUANZA CHALENJI, Z'BAR WAMTIMUA KOCHA MKUU

SIKUI chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Chalenji, Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA), kimemtimua kocha  mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes', Stewart John Hall, imefahamika.
Sababu ya kutimuliwa kwa Hall ambaye pia ni kocha wa timu ya Soka ya Azam ya jijini Dar es Salaam imeelezwa ni kutokana na kushindwa kujiunga na kambi ya timu hiyo iliyopo nchini Misri.
Kwa mantiki hiyo, Zanzibar Heroes sasa itaendelea kunolewa na Mmisri Abdelfatah Abbas  na Hemed Morocco.
Zanzibar Heroes imepiga kambi nchini Misri kujiandaa na michuano ya Chalenji inayotarajiwa kuanza jumamosi katika dimba la Taifa, jijini Dar es Salaam, ambapo Zanziba ipo kundi B pamoja na timu za Uganda, Burundi na Somalia.

Comments