SANTO AENDA ASIA, DERICK WALULYA KUJAZA NAFASI YAKE

Klabu  ya Simba imekubaliana na ombi la mchezaji wake Jerry Santo aliyeomba aruhusiwe kwenda barani Asia kucheza soka la kulipwa mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa na Simba mwezi huu.
Simba inamtakia heri na fanaka mchezaji huyo kwenye maisha yake ya kisoka.
Nafasi ya Santo itajazwa na mchezaji kutoka nchini Uganda, Derick Walulya, (pichani) ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA).

Comments