NIZAR KHALFAN ASAJILIWA PHILADELPHIA UNION

BAADA ya kutemwa na klabu ya soka ya Vancouver Whitecaps ya CAnada, kiungo wa Tanzania , NIzar Khalfan amepata ulaji mwingine baada ya kusajiliwa na klabu ya Philadelphia Union inayoshiriki ligi kuu ya nchini MArekani.
Pamoja na kumtema huko, kocha wa Vancouver Rennie alisema alikuwa na wakati mgumu katika kutoa maamuzi hayo kwania kiungo huyo alionyesha kiwanbgi cha juu katika kipindi cha mwisho cha mkataba wake.
Hata hivyo, kocho alifurahi kusiki nyota huyo ambaye pia anaichezea timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kupata timu nyingine ya kuichezea.

Comments