MSONDO NGOMA, SIKINDE KUONYESHANA KAZI KRISMAS


Na Mwandishi Wetu
Bendi pizani za Msondo Ngoma na  Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae)  zitapambana siku  ya sikukuu ya Krismasi mwaka huu kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Temeke.
Mpambano huo umeandaliwa na kampuni za Bob Entertainment na Keen Arts na kudhaminiwa na kinywaji cha Konyagi.
Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilolitakuwa la funga mwaka na kuamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wawili wa muziki wa dansi nchini kwa mwaka 2011.
Kapinga alisema ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa, hasa kwenye upangiliaji wa milio ya vyombo, kila bendi itatumia jukwaa lake kwa kupiga kwa muda wa saa moja kabla ya nyingine kupanda jukwani.
“Litakuwa pamabano la aina yake ukizingatia kuwa itakuwa ni mara ya kwanza kwa bendi hizi pinzani kupambana siku ya sikukuu ya Krismasi tangu zianzishwe” alisema Kapinga.
“Pia itakuwa ni mara ya kwanza kwao kushindana katika wilaya ya Temeke ambao ndiyo inaongoza kuwa na wapezi wao.”
Kwa kawaida Msondo Ngoma hufanya maonyesho yao kila Jumamosi kwenye viwanja vya TCC Club, Chang’ombe wakati Sikinde hufanya maonyesho yao kwenye viwanja hivyo hivyo siku ya Jumapili.
Kapinga alisema kampuni yake inafanya mipango ya kuwasafirisha wapenzi wa bendi hizo kutoka mikoa ya karibu kuja Dar es Salaamkushuhudia mpambano huo ambao pamoja na kusherehekea sikukuu ya Krismasi pia utakuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya kinywaji cha Konyagi.

Comments