MRWANDA KUREJEA NYUMBANI?

MSHAMBULIAJI wa Tanzania anayekipiga klabu ya DT Long An Vietnam, Danny Mrwanda huenda akarudi kuichezea timu yake ya zamani, Simba katika mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara na michuano ya kimataifa.
Habari kutoka Simba zinaeleza kuwa mazungumzo baina ya Mrwanda Simba yanakwenda vema kwani mchezaji huyo ameshamaliza mkataba wake wa kuichezea timu hiyo hivyo kinachosubiriwa ni barua ya uthibitisho.
Simba imeamua kumrejesha Mrwanda kundini ili kuziba pengo katika nafasi ya ushambuliaji baada ya wachezaji kadhaa wa idara hiyo kupelekwa kwa mkopo katika timu nyingine.

Comments