MORALI YA WACHEZAJI IPO JUU-JULIO

SIKU chache kabla ya kuanza kwa michuano ya CECAFA Chalenji 2011, kocha msaidizi wa Kilimanjaro Stars, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amejinasibu ya kufanya vema zaidi katika michuano hiyo kutokana na wachezaji wake kuwa na morali ya hali ya juu.
Julio amesema kuwa, kadiri siku zinavyosonga kuelekea mashindano hayo wachezaji wake wamekuwa wajibidiisha zaidi na kutambua kuwa wanakabiliwa na michuano muhimu.
"Kwa kweli morari ya wachezaji wangu ipo juu, hivyo kwa hali ilivyo nina uhakika tutalibakisha tena kombe,"Alisema.

Comments