MILOVAN KUSAINI MKATABA SIMBA KESHO

KOCHA Mserbia Milovan Cirkovic anatarajiwa kutua usiku wa leo, ambapo kesho atasaini mkataba wa kuinoa klabu ya soka ya Simba.
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' amesema kila kitu kuhusiana na mkataba wa kocha huyo kitawekwa hadharani hiyo kesho.
Milovan aliyepata kuinoa Simba mwaka juzi kabla ya kuikacha, anakuja kurithi mikoba ya Mzambia, Moses BAsena ambaye ameshindwa kuiweka katika hali ya kuridhisha timu hiyo alipoiona katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania Bara na kumaliza ikiongoza kwa pointi 27.

Comments