MICHUANO YA CECAFA CHALENJI KUANZA LEO, VIINGILIO HIVI HAPA

MICHUANO ya kombe la CECAFA Chalenji 2011 inatarajiwa kuanza leo, ambapo kutakuwa na mechi mbili za ufunguzi, Burundi itacheza na Somalia, Uganda itacheza na Zanzibar.

Viingilio kwa mechi za hatua ya makundi kwa michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza leo (Novemba 25 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam vitakuwa kama ifuatavyo;
Kwa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo ni zaidi ya 30,000 kiingilio kitakuwa sh. 1,000 wakati viti vya rangi ya chungwa ambavyo ni zaidi ya 10,000 kiingilio kitakuwa sh. 3,000. VIP C na B ambayo jumla ya viti vyake ni 8,000 kiingilio kitakuwa sh. 5,000 wakati VIP A yenye viti 700 kiingilio ni sh. 10,000.

Comments

  1. Asante kwa kutupa taarifa za hiyo michuano, na je hizo mechi zitaanza mda gani?
    na pia kwa watanzania wenzangu mnaweza kupata links mbalimbali za michezo na zinginezo za kitanzania kupitia http://www.tanzaniakwetu.com

    ReplyDelete

Post a Comment