MGOSI ASHINDWA KUIFUNGUKIA YANGA

MSHAMBULIAJI aliyepata kutikisa katika klabu ya Simba, Mussa Hassan Mgosi ambaye kwa sasa anakipiga kwa ridhaa katika klabu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya KIdemokrasia ya Congo, amegoma kuzungumzia mpango wake wa kujiunga kwake na klabu ya Yanga.

Hatua hiyo imnafuatia kuwepo kwa tetesi za Mgosi kuwa mbioni kusajiliwa na Yanga kwa ajili ya kuitumikia katika mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.
Mfungaji huyo bora wa zamani wa ligi kuu bara, kwa sasa yupo nchini akiitumikia timu ya Taifa ambayo ipo kambini kujiandaa na michuano ya Cecaf Chalenji inayotarajiwa kuanza keshokutwa, jijini Dar es Salaam.

Comments