KIM POULSEN ATANGAZA SILAHA ZA COSAFA HUKU AKIMTEMA ULIMWENGU

KOCHA wa za vijana, Kim Poulsen akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na kikosi cha timu ya Vijana wenye umri chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’itakayoshiriki michuano iliyoandaliwa na BAraza la Vyama vya soka Kusini mwa Afrika (COSAFA) inayotarajiwa kufanyika  Gaborone, Botswana kuanzia Desemba Mosi.KUshoto ni ofisa habari wa TFF Boniface Wambura, ambapo Ngorongoro itaondoka Novemba 30  huku Poulsen, akiwatema wachezaji wake mahiri, Thomas Ulimwengu na Ibrahim Juma katika kikosi chake.



Wachezaji hao wameachwa kutokana na kuzitumikia timu za Taifa ambazo kwa sasa zipo katika maandalizi ya michuano ya Chalenji inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi, Novemba 25 jijini Dar es Salaam ambapo Ulimwengu ameitwa kikosi cha Bara ‘Kilimanjaro Stars’ huku Ibrahim akiitwa Zanzibar Heroes.
Wachezaji watakaounda kikosi hicho kuwa ni pamoja na Saleh Malande (Simba), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Suagr), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Said Samir (Kagera Sugar), Samuel Mkomola (Azam), Frank Domayo (JKT Ruvu Stars) na Omega Seme (Yanga0.
Wengine ni Atupele Green (Yanga), Jerome Reuben (Moro United), Simon Happygod (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Abdallah Hussein (AFC), Rajab Mohamed (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba), Emily Josiah (TSC Mwanza), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting Stars).
Ngorongoro Heroes ambayo iko kundi D itaanza kampeni hizo Desemba mosi kwa kukipiga na Zambia, kabla ya kucheza nma Afrika KUsini Desemba 4 na kisha kukwaana na Mauritius Desemba 6.

Comments