MASHABIKI WA YANGA KAENI MKAO WA KUPATA MAMBO YA UKWEHEEE

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga wamefungua Website kwa ajili ya Mashabiki wanaotaka kujua historia ya timu hiyo.
Ofisa habari wa Yanga Luis Sendeu amesema kuwa Klabu hiyo ina wapenzi wengi sana lakini hawajui vizuri historia yake hivyo kufungua Website hiyo kutasaidia kupata taarifa zake.
Alisema kuwa Website hiyo kwa sasa iko katika hatua za mwisho kukamilika na kuwa hadi wiki ijayo itakuwa rasmi.
Sendeu alisema kuwa Mashabiki wa Yanga ambao wako nje ya Tanzania wamekua wakisumbuka sana kupata taarifa za Klabu kutokana na kutokua na mtandao utakaowawezesha kupata taarifa.
“Yanga ina Mashabiki Uingereza,Kenya na nchini nyingine walikuwa wanataka taaraifa za timu na klabu kwa ujumla lakini walikua wanakosa hivyo Website hii itawasaidia sana”alisema Sendeu.
Alisema kuwa mbali na kujua historia ya Klabu hiyo Mashabiki watapata nafasi ya kujua wachezaji wa timu hiyo na Viongozi kwa ujumla.

Aliitaja Website hiyo kuwa ni http://www.youngafricans.co.tz/ na kuwa ambapo aliwataka watu wanaotaka kutangaza biashara zao wajitokeze wawze kutangaza.

Comments