MAMA ZAKHIA BILAL ALIPOZINDUA KUNDI LA T-MOTO MODERN TAARAB USIKU WA KUAMKIA LEO

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akivuta utepe kuzindua rasmi kundi jipya la Taarab la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) ‘Real Madrid’ wakati wa uzinduzi wa kundi hilo na albam ya kwanza ya kundi hilo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jana usiku.

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akipokea zawadi ya Cd za kundi la T-Moto, kutoka kwa Mkurugenzi wa kundi hilo, Amin Salmin, baada ya Mama Zakhia kuzindua rasmi kundi hilo jana usiku kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Mkurugenzi wa Kundi la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) ‘Real Madrid’, Amin Salmin, akizungumza jukwaani wakati wa uzinduzi wa kundi hilo, uliofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Msanii wa kundi la Tanzania Modern Taarab, Jokha Kasim,  akiimba jukwaani kibao chake cha Unavyojidhan Haufanani, wakati wa uzinduzi wa Kundi na  albam ya kwanza ya kundi hilo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam jana usiku Nov 4.

 Msanii wa kundi la Tanzania Modern Taarab, Bi Mwanahawa Ally, akiimba jukwaani kibao chake cha Aliyeniumba Hajanikosea, wakati wa uzinduzi wa Kundi na  albam ya kwanza ya kundi hilo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam jana usiku Nov 4
Mama Zakhia Bilal, Mama Tundu Pinda, Mama Kawawa, wakiwa katika picha ya pamo wasanii wa kundi la T-Moto baada ya kuzinduliwa rasmi.

Msanii wa kundi la Tanzania Modern Taarab, Mosi Suleiman, akiimba jukwaani wakati wa uzinduzi wa Kundi na  albam ya kwanza ya kundi hilo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam jana usiku Nov 4.

Msanii wa kundi la Tanzania Modern Taarab, Mrisho Rajab, akiimba jukwaani kibao chake cha Mchimba Kaburi Zamu yake Imefika, wakati wa uzinduzi wa Kundi na  albam ya kwanza ya kundi hilo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam jana usiku Nov 4.

 Waimbaji wa bendi ya Mapacha Wa3 kutoka (kushoto) Kalala Junior, Jose Mara na Khalid Chokoraa, wakishambulia jukwaa wakati walipokuwa wakisindikiza uzinduzi wa Kundi la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jana usiku Nov 4.

Mamapipiro na mama Sufiani Mafoto nje ya ukumbi wa Diamond Jubille jana baada ya onyesho la uzinduzi wa kundi la Tanzania Modern Taarab 'T-Moto'

Picha zote kwa hisani ya www.sufianimafoto.blogspot.com

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHNovember 6, 2011 at 8:33 PM

    AAAH MAMA PIPIRO NAKUONA HAPO...KWELI DAR MCHANA NDOGO USIKU KUBWA!!

    MDAU WA BOMBA US

    ReplyDelete

Post a Comment