MALAWI YAALIKWA KOMBE LA CECAFA

SHIRIKISHO la soka Afrika Mashariki na  Kati (CECAFA) limeialika timu ya Malawi kushiriki michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi  Novemba 25 hadi Desemba 10, jijini Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa leo na Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye alipotangaza ratiba ya makundi ya michuano hiyo iyakayoshirikisha timu 11.
“Tumeialika timu hii makusudi kwa nia ya kusisimua maendeleo ya soka katika ukanda huu. Ni matumaini yetu kuwa timu hii italeta changamoto katikamichuano hiyo na kuifanya iwe na ushindani mkubwa,” Musonye amekaririwa akisema.
"Ni lengo la CECAFA kuona mpira wa miguu katika ukanda huu unakuwa wa kiwango cha juu kabisa. Na timu mojawapo katika ukanda huu ituwakilishe katika kombe la Dunia huko Brazili mwaka 2014,"Alisema.
Mwaka huu timu ziakazoshirikini  Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Djibouti, Somalia, Ethiopia, Sudan, Tanzania, Zanzibar, Eritrea.
Kampuni ya bia yaSerengeti inapata heshima ya kuwa mdhamini mkuu na kupata hakimiliki ya kutumia nafasi hii kutangaza bidhaa yaTusker kipindi chote cha mashindano hayo.
Kundi A-Tanzania Bara,Rwanda,Ethiopia na Djibouti, Kundi B-Uganda,Burundi,Zanzibar na Somalia, Kundi C-Sudan,Kenya,Malawi na Eritrea

Comments