LICHA ya kumaliza mkataba wake na Kongsvinger ya Norway, Nahodha wa Stars Henry Joseph amesema hana mpango wa kurejea kuvitumikia vilabu vya nyumbani. 
Henry aliyekuwa akiichezea Simba kabla ya kutimkia huko, alisema anachoangalia ni kujiendeleza zaidi ili aweze kupata timu zitakazompa maslahi bora zaidi.
Alisema anafurahi kuona klabu nyingine za Ulaya zikitaka kumsajili hivyo kwa sasa anaangalia ni wapi kutalapokuwa na manufaa kwake na kwenda kujiunga.

Comments