KUZIONA STARS, CHAD BUKU 2

WAKATI timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ikitarajiwa kutua kesho kwa kishindo ikitokea jijini N’Djamena,Chad baada ya kuwatandika mwenyeji mabao 2-1, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeanika viingilio vya mechi yao marudiano itakayopigwa keshokutwa katika dimba Taifa, ambapo kiingilio cha chini kimepangwa kuwa shilingi 2,000.

Stars na Chad zitakwaana katika mechi hiyo ya marudiano ya kuwania kufuzu kucheza makundi ya kombe la Dunia ambayo fainali zake zitapigwa nchini Brazil mwaka 2014.
Kaatibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alimesema  kuwa viingilio hivyo vimepangwa ili kuwapa fursa Watanzania wengi hasa mashabiki wa soka kuweza kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hiyo ambayo ambayo inahitaji sare yoyote ili kuvuka hatua ya pili.
Alisema, kiingilio cha juu katika mchezo huo kitakuwa sh. 20,000 Kwa mashabiki watakaokaa jukwaa la VIP A, VIP B, sh. 10,000, VIP C sh. 5,000 huku jukwaa la Orange kikiwa sh. 3000.

Comments