KIPIGO ZANZIBAR HEROES...KOCHA ALILIA NYOTA WAKE

WAKATI kesho  inashuka katika dimba la Taifa kutupa karata yake ya pili katika michuano ya Chalenji, kocha mkuu wa timu hiyo Mmisri Mohammed Morocco amesema kuanza vibaya kwa timu yake kwenye michuano hiyo kunatokana na timu kukosa maandalizi ya pamoja.
Morocco ambaye kikosi chake leo kinakwaana na Burundi, alisema hayo juzi mara baada ya kumalizika mechi baina ya Zanzibar na Uganda ambapo timu yake ilambulia kipigo cha mbao 2-1.
Alisema, licha ya timu yake kucheza vizuri katika mechi hiyo, kilichopelekea timu yake kukosa ushindi ni wachezaji kutocheza kitimu kwani baadhi yao hawakuwepo katika kammbi ya maandalizi iliyokuwa nchini Misri.
“Timu yetu ilicheza vizuri lakini tatizo lilikuwa ni kutocheza kitimu, lakini nitakifanyia marekebisho katika mechi inayofuata ili ushindi upatikane,”Alisema.
Kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, timu hiyo ilipiga kambi nchini Misri ambapo iliwakosa nyota wake wanne wakiwmo Nadir Haroub Cannavaro, Agrey Morris, Nassor Said 'Cholo' na Mwadin Ally ambao walikuwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Stars ilikuwa na kibarua cha mechi ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya kombe la dunia dhidhi ya Chad, ambapo ilifanikiwa kusonga mbele.
Nyota hayo walishindwa kuungana na wenzao baada ya kukosa viza za kuwawezesha kuingia nchini humo kwa madai kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilizuia pasi za kusafiria za wachezaji ambapo viongozi wa chama cha soka Visiwani Zanzibar (ZFA) waliwaomba TFF iwapatie pasi hizo bila mafanikio.
Kabla ya mechi hiyo ya Zanzibar na Burundi, kutatangulia mechi baina ya Namibia dhidi ya Djibout.

Comments