KILIMANJARO BOYS YARARURIWA NA AMAVUBI MBELE YA PINDA




WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, leo ameshuhudia kipigo cha bao 1-0 ilichokipata Timu ya Taifa ya Bara ‘Kilimanjaro Boys’ dhidi ya Rwanda ‘Amavubi’.
Katika mechi hiyo ya kuwania michuano ya Cecafa Chalenji ambapo Kili Boys ni mabingwa watetezi, Pinda alikuwa mgeni rasmi ambapo kabla ya kushuhudia mechi hiyo alifungua rasmi michuano hiyo.
Rwanda walijibu mashambulizi dakika ya tano kupitia kwa Mugiraneza Jean Baptist lakini shuti lake likapanguliwa na Kaseja, dakika ya 16. almanusura Rwanda walikise nyavu za Stars kupitia kwa Bayisenge Emery aliyepiga shuti kali langoni mwa Stars ambalo halikuzaa matunda.
Dakika 24 Kalekezi Olivier aliwainua vitini mashabiki wa Amavubi baada ya kuwachambua mabeki wa Kili Boys na kupiga shuti lililotinga katika nyavu za Kili Boys.
Katika mchezo huo, Kili Boys iliwatoa Ibrahim Mwaipopo, Haruna Moshi na Mbwana Samatta na kuwaingiza Juma Jabu, Thomas Ulimwengu na Musa Mgosi, wakati Rwanda iliwatoa Kalekezi Olivier, Tibingana Charles na kuwaingiza Bakota Kamana na Eranza Jean
Kili Stars:Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Ibrahim Mwaipopo/Juma Jabu, Said Morad, Juma Nyoso, Shaban Nditi, Mrisho Ngasa, Nurdin Bakari, Mbwana Samatta/Musa Mgosi, Haruna Moshi/Thomas Ulimwengu na Ramadhan Chambo.
Amavubi:Ndori Jean Claude, Kalekezi Olivier, Ndaka Frederick, Gasana Erick, Nshutiyamangara Ismail, Tibingana Charles, Ngabo Albert,Mungiraneza Jean Baptist, Haruna Niyonzima, Bateera Andrew na Kagere Meddie.

Comments