JUMA JABU KUITALIKI SIMBA?

BEKI mahiri wa Wekundu wa Msimbazi, Juma Jabu 'JJ' huenda akaitaliki timu hiyo iwapo mpango wake wa kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini utafanikiwa.

Jabu ambaye mkataba wake Simba unamalizika mwezi Desemba mwakani kwa sasa amkekaa mkao wa kula kusubiria majibu yake toka kwa wakala anayemfanyia mipango, Yussuf Bakhressa.

Comments