JULIO AOMBA RADHI, AAHIDI MAKUBWA LEO

KOCHA msaidizi wa timu ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Boys', Jamhuri Kihwelo 'Julio' amewaomba radhi Watanzania kutokana na timu yake kuanza vibaya kwenye michuano ya Chalenji ambapo juzi ilitandikwa bao 1-0 na Rwanda 'Amavubi'.
Julio alisema kwamba kipigo hicho kilitokea kwa bahati mbaya hivyo amekifanyia marekebisho kikosi chake na kuahidi kuwa kitafanya vema leo dhidi ya Djibout.

Comments