JULIO AMKEJELI SMG

KOCHA msaidizi wa Kilimanjaro Stars, Jamhuri Kihwelo 'Julio' ametoa kauli inayoonyesha kumkejeli mshambuliaji wa zamani wa Yanga anayecheza soka la kulipwa nchini Angola, Said Maulid 'SMG'.
Mambo yalikuwa hivi:Mara baada ya kutangaza kikosi cha timu hicho juzi katika ofisi za TFF, waandishi walihoji baadhi ya wachezaji wanaoona ni wangefaa kuwepo kundini, huku wakimtaja SMG kudai kuwa yupo tayari kuitumikia timu hiyo.
Lakini Julio akitoa kauli iliuoonekana ni kejeli alisema"Haya andikeni na SMG ameitwa Stars, aje aungane na wenzake katika mazoezi jama akiwa bora tutamchagua kwenye kikosi cha wachezaji 20,"Alisema.
Julio alitangaza nyota 28 watakaunda kikosi hicho na kusema kwamba watapunguzwa na kubaki 20.

Comments