ERITREAYAJITOA CHALENJI, NAMIBIA WAZIBA PENGO


Namibia itashiriki michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza Novemba 25 mwaka huu ikiwa timu mwalikwa baada ya Eritrea kujitoa. Hivyo Namibia inaingia moja kwa moja katika kundi A ambalo lina mabingwa watetezi Tanzania Bara, Rwanda na Djibouti.
Pia ratiba ya mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia ya Tusker imetangazwa rasmi leo (Novemba 16 mwaka huu) ambapo mechi zote zitachezwa Dar es Salaam baada ya Mkoa wa Mwanza kushindwa kutimiza masharti iliyopewa ili nayo iwe kituo cha michuano hiyo.
Mechi mbili zitachezwa kwa siku Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam isipokuwa Novemba 26 mwaka huu ambapo kutafanyika uzinduzi rasmi saa 10 jioni kwa mechi kati ya Tanzania Bara na Rwanda.
Novemba 25 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Burundi na Somalia (saa 8 mchana) na Uganda na Zanzibar itakayoanza saa 10 jioni.

Comments