CANNAVARO, BABI KUTIMKIA MISRI KESHOKUTWA

NYOTA wanne wanaokipiga katika timu ya Taifa, NAdir Haroub 'Cannavaro', Abdi Kassim 'Babi', Mwadin Ally na Agrey Morris wanatarajiwa kwenda nchini Misri keshokutwa kujiunga na wenzao timu ya Taifa ya zanzibar 'Zanzibar Heroes' ambayo imepiga kambi huko kujiandaa na michuano ya Chalenji.
Wachezaji hao watakwenda huko mara baada ya kuitumikia Stars inayokabiliwa na mechi ya kuwania kufuzu michuano ya awali ya kombe la Dunia djhidi ya Chad leo.
Tayari kikosi cha Zanzibar Heroes kipo huko kwa siku kadhaa kikijiandaa na michuano ya Chalenji inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 25 hadi 10 jijini Dar es Salaam, huku  timu nyingine zinazotarajiwa kushiriki ni pamoja na Tanzania Bara, Uganda, Kenya, Sudam, Eritrea, Djibout, Rwanda, Ethiopia na Malawi.

Comments