CANAVARO NA WENZAKE WAKWAMA KWENDA MISRI

NYOTA wanne walioitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes' wanaocheza Tanzania BAra wakiwmo Nadir Haroub Cannavaro, Agrey Morris, Nassor Said 'Cholo' na Mwadin Ally wameshindwa kwenda Misri kuungana na wenzao wanaojiandaa na michuano ya Chalenji inayotarajiwa kuanza Novemba 25 jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo inafuatia kukosa viza za kuwawezesha kuingia nchini humo baada ya TFF kuzuia pasi za kusafiria za wachezaji hao pindi walipokuwa wanaitumikia timu ya Taifa iliyokuwa inakabiliwa na mechi ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya kombe la dunia dhidhi ya Chad, jumatano iliyopita na Stars kusonga mbele.
Imeelezwa kuwa viongozi wa ZFA walikuwa wakiwaomba TFF iwapatie pasi hizo bila mafanikio na hata baada ya mechi hiyo ya marudiano na Chad, waliendelea kupiga danadana na matokeo yake wachezaji hao kukwama.

Comments