20% AKAMATWA NA GRAMU 20 ZA BANGI

MSANII wa bongo fleva aliyeweka historia ya kupata tuzo tano za muziki za Kili mwaka 2011, Abas Hamis Kinzasa maarufu kama 20% anatarajiwa kufikishwa mahakamani Desemba 28, mkoani Lindi baada ya kukamatwa na Bangi.
Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi toka mjini Lindi zinasema kuwa, msanii huyo alikamatwa na bangi hizo siku ya Novemba 10 alipokuwa Kilwa akielekea katika mikoa ya Kusini kwa ziara ya kimuziki.Msanii huyo yupo nje kwa dhamana ya shilingi 500,000.

Comments