ZITTO KABWE, AMOS MAKALLA WAULA SIMBA SC

                                                                              ZITTO
MAKALLA




MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kamwe na  Mbunge wa Mvomero Amos Makala ni miongoni mwa wajumbe wapya wa klabu ya Simba ambao walioteuliwa katika kamati ya utendaji ya klabu hiyo.
 Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Rage, alisema kuwa kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika Jumamosi ya Oktoba 15 imefanya mabadiliko katika kamati mbalimbali.
Alisema katika kamati hizo imewateuwa katika nafasi mbalimbali wanachama wa klabu hiyo ambao wapo kwenye kundi maarufu la Marafiki wa Simba (Friends of Simba) ambapo walikaa pamoja na kuondoa tofautizao zilizokuwa zimejitokeza ili kuleta mafanikio katika klabu yao.
KAMATI YA FEDHA:
Mwenyekiti: Geofrey Nyange 'Kaburu' makamu mwenyekiti Adam Mgoyi, huku wajumbe wakiwa ni Said Pamba, Juma Pinto na Zitto Kabwe.
KAMATI YA MASHINDANO:
 Mwenyekiti: Joseph Itang'are, Azim Dewji ni  Makamu Mwenyekiti,Wajumbe ni Jarry Ambe, Swedy Nkwabi, Hassan Hasanoo,Mohamed Nassor, Richard Ndasa na Suleiman Zakazaka.
KAMATI YA UFUNDI:
Mwenyekiti:Ibrahim Masoud, Makamu Mwenyekitini  Evance Aveva, Wajumbe Danny Manembe, Khalid Abeid, Musley Luwey, Mulamu Nghambi, Said Tuli, Rodney Chiduo, Patrick Rweyemamu.

KAMATI YA USAJILI:
Mwenyekiti:Zakaria Hans Poppe, Makamu wake mwenyekiti Kassim Dewji, Wajumbe ni Francis Waya, Crecensies Magori, Salim Abdallah, Collins Fransch na Gerald Lukomay.

KAMATI YA NIDHAMU: ipo chini ya Peter Swai, Jamal Rwambo, Charles Kenyela, Evody Mmada na Chaurembo.
Rage alisema kamati hizo zimeanza kazi zake mara moja kwa kuwa kila mjumbe tayari ameshakabidhiwa barua yake.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHOctober 17, 2011 at 11:46 PM

    YANI KD WAMEMUWEKA KWENYE KAMATI YA USAJILI BADALA YA MASHINDANO...HALAFU KWENYE KAMATI YA UFUNDI WAMETUMIA VIGEZO VIPI KUMUWEKA MLAMU?MLAMU ALITAKIWA KWENYE KAMATI YA USAJILI,CHIDUO ALIPASWA KUWA MWENYEKITI WA KAMATI YA UFUNDI HUYO NDIO INJINI YA SIMBA KWENYE MAMBO YA UVUMBUZI WA VIPAJI NA MTU WA MPIRA WAKWELI KWANI MPAKA USWAHILI KWENYE MECHI ZA MCHANGANI UTAMKUTA,AMOS MAKALA KAMATI YA FEDHA SAWASAWA AMEKUA AKIWASAIDIA WANYAMA KITAMBO KIMYA KIMYA TOKA AKIWA MWEKA HAZINA WA CCM,ZITTO SINJUI SAWASAWA KWENYE MPIRA I CAN'T COMMENT ON HIM,PATRIC RWEYEMAMU UFUNDI SIJUI BWANA JAPO MWENYEWE NIKIONGEA NAE KWA SIMU ANASEMA SIJUI ANA CHETI CHA AWALI CHA UKOCHA LAKINI HAJAWAHI KUCHEZA MPIRA ZAIDI YA KUCHEZA KIKAPU JAPO ANADAI ALIWAHI KUWA GOLIKIPA SINA KUMBUKUMBU HIZO ZAIDI YA KUMJUA KWENYE KIKAPU,NAWAACHIA WENYEWE WANYAMA,I JUST SAYING

    ReplyDelete

Post a Comment