YUSUF MANJI KUREJEA TENA KUIFADHILI YANGA

HALI mbaya ya kifedha inayoikabili klabu ya soka ya Yanga imeupelekea uongozi wa klabu hiyo kumpigia magoti aliyekuwa mfadhili wa timu hiyo, Yusuf Mehboob Manji ili arejee kuifadhili klabu hiyo.
Msemaji wa Yanga Louis Sendeu amesema leo kwamba maadhimio ya kumuangukia Manji yamepitishwa na uoongozi ambapo wanasubiri arejea kutoka nchini Marekani ili kuweza kuendelea na mchakato huo.
"Tumeshaanza mazungumzo na Manji ambayo yapo katika hali nzuri, lakini kila kitu kitakuwa wazi pindi atakaporejea kutoka Marekeni,"Alisema.
Manji alijiondoa kuidhamini klabu hiyo kutokana na msigano uliotokea baina yake na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo.

Comments