YONDAN RUKSA KUVUNJA MKATABA-SIMBA

UONGOZI wa klabu ya Simba umesema upo tayari kuvunja mkataba na beki wake, Kelvin Yondan kwani inaonekana amechoka kuichezea klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema kwamba anashangazwa na utovu wa nidhamu alionao mchezaji huyo kwani pamoja na vitendo hivyo, uongozi umekuwa ukimuita mara kwa mara kwa ajili ya kutoa maelezo lakini amekuwa akiwagomea.
Alisema wamekuwa wakikerwa na tabia yake ya kuzungumza hovyo na vyombo vya habari badala ya kwenda kuzungumza ili kujua tatizo ni nini na kama atahitaji kuondoaka katika timu hiyo milango ipo wazi."Kama kuna klabu inayomuhitaji ruksa kumchukua ili mradi tu ifuate taratibu, hatuna hiyana naye kama atatataka kuvunja mkataba tupo tayari pia,"Alisema Rage.

Comments