YANGA YASHINDA 4-2

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga, imepaa hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo kufuiatia ushindi wa mabao 4-2 iliyoupata dhidi ya Toto Africans ya Mwanza, katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo.
Yanga imekwaa nafasi hiyo baada ya kufikisha pointi 18, lakini huenda kesho wakashushwa iwapo Azam itashinda mechi yake dhidi ya Polisi Dodoma.
Mabao ya Yanga leo yalipachikwa na Kenneth Asamoah ambaye alifunga mawili, huku Jerry Tegete na haruna Niyonzima kila mmoja akifunga bao moja.

Comments