YANGA YAKIRI DENI LA HOTELI ALIYOKUWA AKIKAA KOCHA TIMBE

SAM TIMBE
UONGOZI wa klabu ya soka ya Yanga umeahidi kulipa deni shilingi mil.19.5 kwa hoteli moja iliyopo Msasani jijini Dar es Salaam ambayo aliyekuwa kocha wao mkuu Sam Timbe alikuwa anakaa.
Hatua hiyo inafuatia uongozi wa hoteli hiyo kushikilia hati ya kusafiria ya kocha huyo mpaka pale uongozi utakapolipa deni hilo lililolimbikizwa kuanzia mwezi juni.
Msemaji wa Yanga, Lous Sendeu amekiri kuwapo kwa deni hilo na kusema kuwa uongozi unashughulikia suala hilo.

Comments