YANGA YAIPUMULIA SIMBA

MABINGWA wa ligi kuu bara, Yanga  wameanza kuwafukuzia mahasimu wao wa jadi, Simba Simba, baada ya kuifunga Kagera Sugar bao 1-0, kupitia mechi ya ligi kuu bara iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Yanga imepanda hadi nafasi ya tatu kutoka ya Sita baada ya kufikisha pointi 15 na hivyo kuwa nyuma ya Simba inayoshika nafasi ya pili kwenye ligi hiyo kwa pointi 18, huku vinara JKT Oljoro wakiwa na pointi 19.
 Yanga ilipata  bao hilo katika dakika ya 56 kupitia kwa mshambuliaji wake wa kimataifa, Kenneth Asamoah ambaye aliunganisha krosi ya Godfrey Taita.
Asamoah alifunga bao hilo katika kipindi kigumu kwani kipa wa Kagera alikuwa katika harakati za kuokoa hatari langoni kwake, kabla ya shuti la chini la Asamoah lilijaa wavuni.

Comments

Post a Comment