YANGA WAKANA MPANGO WA KUMTIMUA TIMBE

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Yanga wamekanusha kuwa na mpango wa kumtimua kocha wake mkuu Sam Timbe na kumrejesha aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, Costadin Papic.
Msemaji wa Yanga, Louis Sendeu alisema taarifa hizo ni uzushi na zina lengo za kuivuruga klabu yao katika kipindi hiki ambacho hali ni shwari.
Alisema, bado wana mkataba na Timbe na kwamba Papic amekuja nchini kwa masuala yake binafsi.
"Timbe bado ni kocha wetu na ataendelea kuinoa Yanga, Papic amekuja nchini kwa mambo yake, hivyo nawaomba Wanayanga watulie',ALisema.

Comments