VODACO YATANGAZA NJIA ZITAKAZOTUMIKA KATIKA MASHINDANO YA BAISKELI

Meneja Mauzo wa Vodacom kanda ya Ziwa Amos Vuhahula akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza njia zitakazotumika wakati wa mashindano ya  mbio za baiskeli za Vodacom Mwanza Open  Cycle Challenge 2011, zitakazotimua vumbi tarehe 22/10/2011 zitakazoanzia Shinyanga hadi Mwanza na kudhaminiwa na Malta Guinness.


Vodacom Tanzania ambao ni waandaaji wa mbio za baiskeli zijulikanazo kama”Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge” wametangaza njia(route) zitakazotumika kwenye mashindano ya baiskeli ambazo zitaanzia mjini shinyanga na kumalizikia jijini Mwanza tarehe 22 mwezi huu yanayotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 50.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Jijini Mwanza leo, katika ofisi ya Vodacom kanda ya ziwa Meneja Mauzo wa kanda hiyo Amos Vuhahula,alisema kwamba mashindano ya mwaka huu yameboreshwa zaidi ni tofauti na miaka iliyopita kwani njia njia ni ya moja kwa moja ndiyo itakayotumika,ambapo washiriki wataanzia Busanda Mkoani Shinyanga na na kumalizikia Bugando Hill Jijini Mwanza kwa wanaume,wanawake wataanzia Lunele ambapo ni Kilometa 80 mpaka Mwanza na kumalizia Bugando Hill na aliwaomba waendesha baiskeli kujitokeza kwa wingi na kuwaomba wawe makini na utumiaji wa njia(route)ili waweze kupata washindi wa halali na wenye manufaa kwao na wapenzi wa mchezo huu.

Kwa upande wa mbio za walemavu wanawake ambazo ni za kilometa 10 alisema zitaanzia Buhongwa na wanawake wataanzia kona ya Malimbe na kumalizia uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Vuhahula alisema kwa mbio hizo za walemavu wanawake hakutakuwa na kituo cha kuchukulia matunda na maji na badala yake yatawekwa kwenye baiskeli zao katika eneo watakaloanzia mbio hizo.
Aidha kwa upande wa mbio za kilometa 16 zitakazowashirikisha walemavu wanaume pia zitaanzia Buhongwa na kumalizikia uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Vilevile mwaka huu Tanzania bara inasherehekea miaka 50 ya Uhuru,hivyo katika kusherehekea hilo,Vodacom Tanzania ikijua kuwa michezo ni afya,inahamasisha watu wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea kushiriki,yeyote kati ya hao akimaliza mbio wa kwanza ndani ya kundi la watu 50 wa awali,atajipatia shilingi laki 3 kwa wanaume na kwa wanawake itakuwa shilingi laki 2,alisema Meneja huyo.

“Meneja huyo wa mauzo kanda ya ziwa wa Vodacom Tanzania alisema Mbali na haya yote amewahamasisha washiriki kujitokeza na kujiandikisha kwa wingi ili wajipatie zawadi kwenye mbio hizo zitakazoanzia mkoani Shinyanga na kumalizikia jijini Mwanza Oktoba 22 mwaka huu.

Amezitaja zawadi hizo kwa washiriki wa mbio za kilometa 150 mshindi wa kwanza atajipatia shilingi 1,500,000, wa pili kiasi cha 1,000,000, wa tatu 700,000, ambapo mshindi wa nne hadi wa kumi kila mmoja atajipatia shilingi 500,000 kila mmoja.
Kwa upande wa mbio za mita 80 kwa wanawake mshindi wa kwanza pia atajipatia zawadi ya shilingi milioni 1,100,000, wa pili 800,000, mshindi wa tatu 600,000, wakati washindi wa nne hadi wa kumi kila mmoja atazawadia kiasi cha shilingi 350,000 kila mmoja.

Aidha Meneja huyo ameeleza kwamba kwa upande wa mbio za kilometa 15 ambazo zitawashirikisha watu wenye ulemavu alisema washindi wa kwanza wawili kila mmoja atajipatia jumla ya shilingi 500,000.

Kwa washindi wa pili wawili nao watajishindia kiasi cha shilingi 250,000 kila mmoja, washindi wa tatu wawili kila mmoja atapewa kiasi cha 150,000 kila mmoja wakati washindi wa nne wane hadi wa kumi watajipatia kitita cha 100,000 kila mmoja.Na watakaoshika nafasi ya 11 hadi ya 20 katika mbio hizo watazawadiwa kiasi cha shilingi 70,000.
Mbio hizo zimedhaminiwa na Serengeti Breweries kupitia kinywaji chao cha Malta Guinness pamoja na CloudsFm kupitia redio ya watu Vodacom Tanzania pia imekuwa ikidhamini michezo mbalimbali kama vile Soka, Riadha, kuogelea, mashindano ya boti, mashindano ya Mbuzi, Vodacom Miss Tanzania, Tenisi na mingine mingi ili kuhakikisha kwamba taifa linafanya vizuri katika tasnia nzima ya michezo.

Comments