VIONGOZI YANGA NA HOFU YA PAPIC

Na Dina Ismail



LICHA ya Yanga kumkabidhi mikoba ya kuifundisha klabu hiyo, Mserbia Kostadin Papic, uongozi bado unafanya nae mazungumzo ili kukubaliana naye vvitu vya msingi kabla ya kuingia naye mkataba.

Hatua hiyo inafuatia kocha huyo kuwa na matatizo madogomadogo ambayo yalipelekea uongozi kushindwa kumuongeza mkataba miezi kadhaa kabla ya kumalizika, kabla ya kocha huyo kutimka.

Mmoja ya viongozi wa Yanga aliliambia Tanzania Daima kwamba kinachofanyika sasa ni kuzungumza na Papic mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuweka mambo katika mstari ulioonyooka.

“Papic ni kocha mzuri na ndiyo maana tumeridhia arudi, lakini ana mambo fulanifulani yasiyopendeza hivyo tumeona kuna haja ya kukaa na kuwekana sawa kabla ya kuingia naye mkataba,”Alisema.

Papic ambaye alikuwa akiifundisha Yanga msimu uliopita kabla ya kutimkia kwao kabla ya kumaliza mkataba wake, amepewa tena jukumu la kuinoa timu hiyo akirithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa mkuu wa Yanga, Sam Timbe.

Katika hatua nyingine, viongozi wa matati ya Yanga ya mkoa wa Dar es Salaam jana walikuwa na kikao cha pamoja na viongozi wa timu hiyo kwa ajili ya kupanga mikakati ya kushinda mechi yao na Simba Jumamosi.

Ofisa habari wa Yanga. Louis Sendeu alisema jana kwamba kikao hicho kilichofanyika katika makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwa ni na Twiga kilijadili mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuipatia ushindi timu hiyo.

Kwa upande mwingine, Sendeu alisema kuwa maandalizi ya mechi yao na Simba yanaendelea vema ambapo mpaka sasa timu bado inaendelea na kambi yake katika mamako makuu ya klabu hiyo.

Comments

  1. YANGA BOMBA - UHURU BRANCHOctober 27, 2011 at 4:36 AM

    UPUUZI HUU NDIO NISIOUPENDAGA HUYU SENDEU SI ULIMNUKUU JUZI AKISEMA TIMBWE AHONDOKI YANGA NAPAPIC YUKO HUKO BONGO KWA SHUGHULI ZAKE WALA YANGA HAINA MPANGO NAE?????AKAENDA MBALI ZAIDI KWA KUSEMA WANAONEZA "UVUMI" WA PAPIC KUJIUNGA YANGA NI MAADUI WASIOITAKIA MEMA YANGA..LEO BILA AIBU WALA KUOMBA RADHI KWA KUTUPA TAARIFA ZA UONGO ANAKUJA NA SUALA LA MKATABA WA MTU ALIEKUJA DAR KWA SHUGHULI ZAKE BINAFSI!!!HIVI HAWA WANDISHI WENZENU WANA MATATIZO GANI MWANANGU?MAANA HATA YULE MWINGINE ALIEANDIKA BARUA YA KUACHA KAZI SIMBA KWA NJIA YA BARUA PEPE(HII SIJAWAHI KUIONA POPOTE) NAE ALIKUA NA KA UNYANI KAMA HAKA HAKA..

    ReplyDelete

Post a Comment