VIDA MAHIMBO & ALLY REMTULLAH KATIKA UHURU COLLECTON



Na.Mwandishi wetu.

Siku chache zilizopita yamefanyika maonesho ya mitindo ya mavazi ya Swahili Fashion Week nchini Angola (Fashion Business) yaliyobuniwa na mbunifu wa mavazi kutoka Tanzania almaarufu kama Mustafa Hassanali.
Tarehe 22 Oktober 2011 yanafanyika maonyesho ya mavazi nchini Afrika Kusini chini ya udhamini wa kampuni ya Precision Air yanayotambulika kwa jina la AFI Africa Fashion week ambapo Tanzania inawakilishwa na mbunifu Mustafa Hassanali.
Ufafanuzi tunaotaka kuutoa hapa ni kwamba inajulikana kuwa katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru kwa mara ya kwanza mbunifu huyo atazindua chata ya ‘UHURU’ambayo inawakilisha Tanzania ilipopata uhuru mwaka 1961.
Kwa uhakika sio mara ya kwanza kuzinduliwa kwa ‘UHURU Collection’ kumefanywa na mbunifu huyo na katika kuwawekeni wazi chata ya ‘UHURU’ inamilikiwa na Wabunifu Mahiri wa Mavazi VIDA MAHIMBO na ALLY REMTULLA.
Wakizungumzia chata ya ‘UHURU COLLECTION’ wabunifu hao wamesema kuwa kwa mara ya kwanza chata hii ilizinduliwa mwezi February 2011 visiwani Zanzibar.
Nembo hii imesajiliwa na inamilikiwa na VIDA MAHIMBO na ALLY REHMTULLAH chini ya Karisma Fashion Group Limited na ndio maana wakati wa uzinduzi ilijulikana kwa jina la UHURU The African Freedom by ALLY REHMTULLAH na VIDA MAHIMBO, for the young and the old, the daring & the conservative…It’s a brand for us all.
Sio kweli kwamba ‘UHURU COLLECTION’ imebuniwa na Mustafa Hassanali na sio kweli kwamba inazinduliwa mara ya kwanza.
Kwa ufafanuzi huu unapohitaji bidhaa yoyote ya ‘UHURU COLLECTION’ wasiliana na VIDA MAHIMBO au ALLY REHMTULLAH @ duka lake la Slipway Shopping Centre-VIDA MAHIMBO STORE.

Comments