VICTOR COSTA AREJEA DIMBANI

BEKI wa timu ya soka ya Simba Victor Costa ambaye alikuwa nje ya dimba kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na kujiuguza nyama za paja, jana ameanza mazoezi na wenzake.

Costa alipata majeraha hayo akiwa na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ iliyokuwa ikijindaa na mechi yake ya mwisho ya kuwania tiketi ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwakani dhidi ya Morocco wiki iliyopita ambapo Stars ililala kwa mabao 3-1 na Morocco.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Costa alisema anamshukuru mungu kwani katika hali isiyotarajiwa amepona haraka majeraha yake.

Alisema anaamini kadiri siku zinavikwenda hali yake itakuwa imara zaidi hivyo kuweza kuisaidia timu yake katika mechi zake zilizobaki kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Simba  inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 24 inaendelea na mazoezi ya kujiandaa na michezo yake mitatu iliyobaki kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza, zikiwemo JKT Ruvu, Yanga na Moro United.

Comments